GET /api/v0.1/hansard/entries/768092/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 768092,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/768092/?format=api",
    "text_counter": 288,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Spika Naibu wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kumshukuru mwenzangu, Mhe. Melly, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hoja hii. Kabla ya hiyo, ningependa kutoa nafasi hii kumshukuru Rais pamoja na Naibu wake kwa kupatiwa nafasi kuongoza kwa muhula wa pili. Ningependa kuchangia Hoja hii kwa sababu ya barabara zetu. Nashukuru ndugu yangu, Mhe. Melly, kwa kufikiria kuwepo kwa barabara za magari ya dharura ili kuwasaidia watu wetu. Ukija Trans Nzoia County, utaona kwamba barabara kule mashinani si nzuri. Kuna magari, tractor s na pikipiki ambazo zinatumia barabara hizo. Ningependa kuunga mkono nikisema kuwa tunafaa kuwa na Mswada kuhusu mambo haya ya barabara na magari ambayo yanatumia barabara hizi. Vile wenzangu wamezungumza, ni lazima tuwe na usalama wa kutosha katika barabara zetu. Ningependa pia kushutumu kitendo cha mauaji ya kijana mdogo jana."
}