GET /api/v0.1/hansard/entries/768099/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 768099,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/768099/?format=api",
"text_counter": 295,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Rehema Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13275,
"legal_name": "Rehema Hassan",
"slug": "rehema-hassan"
},
"content": "Asante sana Naibu Spika wa Muda and Mhe. Melly. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii. Kabla sijazungumzia barabara zetu, ningependa kujiunga na wanawake wenzangu kutoka Tana River kwa sababu ya visa vya ubakaji ambavyo vimezidi. Nikiwa hapa, ningependa kusema, County Commissioner awajibike ili wanaohusika wachukuliwa hatua kwa sababu tumepoteza mtoto kwa sababu ya ubakaji. Mwingine alipata mimba akajiuwa. Mambo haya yamekua zaidi kwa watu wa Tana River. Nikiunga mkono Hoja hii, ningependa kusema kuwa kabla hatujafikiria service lanes mnazozungumzia, barabara yetu kuu ishughulikiwe. Nikiunga mkono Hoja hii ya barabara, ningependa kusema kuwa sisi katika Tana River, kabla hatujafikia hizo service lanes mnazozungumzia, barabara yenyewe ishughulikiwe. Isikuwe ndio imekaa kama kitega uchumi, kila saa inafanyiwa ukarabati. Tunataka tujengewe barabara nzuri kama wenzetu. Kwa upande wa barabara za magari ya dharura, ninaunga mkono kwa sababu ya boda boda na hao wengine."
}