GET /api/v0.1/hansard/entries/768816/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 768816,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/768816/?format=api",
    "text_counter": 82,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kingara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Asante sana Bw. Spika, kwa kunitambua katika kikao hiki. La kwanza kabisa ni kuwashukuru Wabunge wote, haswa Wabunge wa upande wa Upinzani, kwa kukubali kuja tufanye kazi ile tuliyopewa na wananchi. Katika Kenya yetu, tumeendelea sana. Mambo ya usajili, utoaji na usimamizi wa utangazaji ni vizuri uwekwe laini. Kama munavyojua, nchi zilizoendelea zimepiga hatua kubwa na kuweka viwango vya juu sana ndiyo wasajili wasije wakaigwa na wengine ambao hawajachoka. Kenya ni nchi ambayo imeendelea na ina demokrasia. Vilevile, Wakenya wanataka kula jasho lao. Ni vizuri tutafute mikakati mwafaka na ya uzito tutakayoiga. Hii ni ili tuone waliotumia vipawa vyao na kutoa mambo mazuri wakijiburudisha kimapato. Lazima nao wasimamiwe na sheria yetu. Sheria yetu haiwezi kuchukua mwelekeo mwema iwapo sisi kama Bunge hatutaweka mikakati itakayowachunga. Si hilo tu; ni mambo yote yanayohusu watu walio na vipawa ambavyo vingetumiwa kwa ubaya na wengine; tuone wamesimamiwa na sheria. Katika eneo la kutunga sheria, hawana lingine. Sisi Wabunge, ndio tuko na mwanya, nafasi na mamlaka kutoka kwa wananchi na Katiba yetu kusimamia wale ambao hawana nafasi kuingia katika Bunge na kujisimamia. Wakati mjadala kama huu umeletwa, ni vizuri tujisahau kama watu binafsi. Tuchukue msimamo wa Wakenya wote na kuona watoto wetu na marafiki wakihusishwa katika vipawa vya aina mbali mbali. Kama hakuna mikakati kamili, wengine watatumia jasho lao nao wakapata hakuna matunda. Ndio watu wapate matunda yao, ni sisi Wakenya, haswa Wabunge, tutafute mikakati na uzito wa maneno yale yatatumika katika usajili wa maandishi yoyote yatakayosimamia ujuzi wa Wakenya kwa njia mbali mbali. Ni jambo la busara sana kwa sababu kuna nchi ambazo vipawa vya watu binafsi, haswa muziki na michezo, vimetumiwa na wengine waliokuja kujinufaisha; wanawacha wanaotoa vipawa vile kuwa watu wanyonge. Ili hilo lisiwe la kuigwa hapa Kenya, itabidi sisi na Wabunge wa hapa Kenya tuwe na uzito wa usajili wa maandiko yote yatakayosimamia watu wenye vipawa. Kwa hivyo, Mhe. Spika, nimesimama kuunga mkono. Ningeomba Wabunge wenzangu, Waheshimiwa, waungane na mimi tuunge mjadala huu mkono. Asanteni."
}