GET /api/v0.1/hansard/entries/769650/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 769650,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/769650/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Asante, Mhe. Spika wa Muda. Marekebisho ya pesa ni sawa. Inafaa pesa zitengwe za kuhusika na mambo ya misitu kwa sababu zinapitia vitengo vingi. Kama inawezekana, hizi pesa za misitu zingewekwa katika NG-CDF. Hiyo asilimia mbili katika NG- CDF ni kidogo sana kwa misitu. Misitu lazima tuzingatie. Hiyo misitu ndiyo inasaidia wafugaji kama sisi wenye ng’ombe na mbuzi. Hiyo misitu ikiisha, hata nyasi hatuwezi kupata. Kwa hivyo, NG-CDF ingeongezewa pesa zaidi ya hiyo asilimia mbili ili misitu isaidike. Pia, hatuelewi watu wa misitu wanachunga nini kwa sababu hao ndio wanamaliza misitu. Sio wananchi ambao wanamaliza misitu. Watu wa kuchunga misitu ndio wanamaliza misitu. Wakipata mtu ana makaa, mbao ama miti, wanamnyang’anya na wanampeleka kortini na hiyo miti au makaa haionekani tena. Wao wenyewe wanauza hizo bidhaa. Kwa hivyo, lazima kazi ya hao watu wa kuchunga misitu ijulikane. Wao ndio wanamaliza misitu. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}