GET /api/v0.1/hansard/entries/769756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 769756,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/769756/?format=api",
    "text_counter": 202,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Asante sana Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii inayohusu ulazimishaji wa shule na wananchi kupanda miti. Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, mwanzo, ningependa kumpongeza aliyeleta Hoja hii, Mhe. Chepkut. Kaunti ya Kwale pia imeadhirika sana. Kuna watu kama wawili katika kila eneo letu la Bunge ambao wamekuwa wakipata shida ya njaa. Kukata miti kunapoteza maji maana mizizi ya miti haiwezi kuweka maji kwa muda mrefu. Ukosefu wa maji unasababisha ukosefu wa chakula. Mwaka uliopita kuna sehemu zilikuwa na njaa. Ukosefu wa maji pia unasababisha upungufu wa miti shamba inayotumika kwa kutengenezea dawa ya kienyeji. Hii ni dawa ambayo wananchi na madaktari wamekuwa wakitumia tangu enzi. Ukosefu wa mvua umesababisha upungufu wa aina hii ya miti inayotumika kutengeneza hizo dawa. Iwapo upungufu wa maji utazidi, itakuwa vigumu kuregesha miti ya aina…"
}