GET /api/v0.1/hansard/entries/770040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 770040,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/770040/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "December 7, 2017 SENATE DEBATES 40 Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ningependa pia kujumuika na wenzangu katika kuunga mkono Hoja hii ya irrigation . Mimi nimetoka katika Kaunti ya Tana River ambayo ina miradi mikubwa ya irrigation . Katika maeneo bunge yote tatu ya Kaunti ya Tana River kuna irrigation schemes kama Bura Irrigation Scheme, Hola Irrigation Scheme ambako ninatoka. Tuko pia na Galana Irrigation Scheme ambayo iko upande wa Galana-Kulalu na Tana and Athi Rivers Development Authority (TARDA) upande wa Garsen. Sehemu ambazo ziko na miradi ya Irrigation zikifanya vizuri tutakuwa na chakula cha kutosha hata kuuza. Hii itawezekana tu policy hii ikifanya kazi vizuri na wenye kusimamia miradi hiyo wataziwezesha jamii hizo kufanya mambo ya irrigation vizuri. Wanayofanya irrigation watapata mapato hata mvua isiponyesha kwa sababu kutakuwa na unyunyizaji wakati wowote. Mazoa yatapatikana hata bila mvua kunyesha. Mimi natoka sehemu hiyo na nimezitembelea miradi zote. Mimi pia ni mkulima na mfugaji. Sehemu ambazo zina miradi ya unyunyizaji maji zina s ettlement areas . Watu kutoka sehemu tofauti huja pamoja na urban centres huanza. Katika hali hiyo, wale wanaokuja pamoja wanakaa kama jamii. Katika hiyo jamii utapata vikundi vya watu katika miji mbalimbali katika sehemu za irrigation. Wanapokuwa wengi, mambo ya siasa pia yanatokea. Miradi ya unyunyizaji maji huajiri vijana ambao wanaishi huko na wengine ambao wanatoka sehemu mbalimbali. Wao hufanya kazi tofauti tofauti. Baadhi yao hufanya kazi za ofisi na wengine kazi zingine. Kwa sababu hiyo, Hoja hii inafaa kuungwa mkono kwa wingi. Sehemu ambazo irrigation inafanywa ni mbali na mto. Katika Bura Irrigation Scheme, canal zimetoka mbali na maji yanaenda mbali. Katika hali hiyo, watu ambao wanaishi sehemu kame kabisa wanapata maji. Wanyama wa pori wako katikati ya hizo canals na wanapata maji. Mifugo pia wanapata maji katika hali hiyo. Hili ni jambo ambalo linafaa kuungwa mkono. Kwa sababu hiyo, nami pia ninaunga mkono. Utaona pia jamii zingine zinafanya uvuvi wa samaki katika yale mabwawa yanayopatikana yaliyo hapo. Hali hii inaongeza mapato ya jamii za wavuaji samaki. Bw. Naibu Spika, tukijumlisha yote, utaona mambo ya jamii itakuwa hapa kwa sababu jamii wamekuja pamoja. Mambo ya siasa inakuwa hapo vizuri pamoja na uchumi au mapato yetu pia inaendeshwa vizuri na mambo ya irrigation . Kwa sababu hiyo, nami pia ninaunga mkono hoja hiyo."
}