GET /api/v0.1/hansard/entries/770980/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 770980,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/770980/?format=api",
    "text_counter": 216,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Jukumu la Serikali ni kupitisha sheria na kanuni zitakazofaa ili wenye kustahili ambao ni wenye viwanda nchini wapewe nafasi. Kwa mfano, thamani ya kampuni ya Safaricom ni mabilioni ya pesa. Ilipozaliwa ilikuwa inamilikiwa na serikali. Baadaye ilibinafsishwa. Leo nataka tujiulize swali katika Bunge hili na tulijibu kiukweli ndani ya nafsi yetu: lau Safaricom ingekuwa bado ni mali ya umma, kisha tungojee Rais achague mkurugenzi wake, je, tungekuwa tunailipia madeni na kusema wafanyikazi wake walipwe mishahara? Nia na madhumuni yangu ni kuwasihi wenzangu tusiwe tukiangalia na kusema kila siku Serikali ifanye jambo hili ama lile ama itoe amana. Hata sisi kule Pwani tunayo sekta ya uvuvi na korosho lakini hatujaona Serikali hii ilioko na zile zilizopita zikitufanyia jambo lolote. Tunayo vilevile sekta ya chumvi. Hakuna yeyote anayeweza kuishi bila chumvi. Lakini hatujaona yeyote ambaye amefanya jambo lolote kuhusu sekta hiyo. Kwa nini? Ni kwa sababu kuna watu binafsi wanaoweza kufanya hiyo kazi sawa sawa. Pesa zetu hazitaliwa kiholela."
}