GET /api/v0.1/hansard/entries/771267/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 771267,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/771267/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Makokha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2286,
"legal_name": "Geoffrey Makokha Odanga",
"slug": "geoffrey-makokha-odanga"
},
"content": "Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Huu ni mjadala muhimu. Kwanza ningependa kutuma rambirambi zangu za dhati kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao. Ni jambo la kusikitisha mno kwa sababu hivi juzi, tulikuwa tunajadili kuhusu vile tunavyoweza kupanua barabara zetu. Sehemu hii ya Sachangwan ni sehemu ambayo wananchi watukufu wa Kenya wamepoteza maisha yao kwa muda. Lazima Bunge hili lichukulie hili jambo kwa uzito kwa sababu si vyema tunavyoendelea kupoteza watu wetu muhimu katika nchi hii. Sehemu hii ya Kamukuywa ninapokumbuka, ni sehemu ambayo nimesomea. Ni sehemu ambayo watu wengi wamepoteza maisha yao. Si jambo geni kwa Serikali kuu. Lazima kuna mtu ama watu ambao wamelala katika kazi yao. Kama vile wenzangu wamesema, tunapitisha sheria hapa, tunakaa muda mrefu tukijadili juu ya sheria lakini sheria hii haifuatiliwi na wale wanaohusika. Kwa hivyo ni wakati ambapo lazima wale wanaohusika, wafuatilie na kuhakikisha ya kwamba sheria inapopitishwa, inafanya kazi na waamuke kutoka kwa usingizi. Si vyema kupitisha sheria ambayo haifanyi kazi na haisaidii Mkenya wa kawaida. Ni jambo la kusikitisha. Sehemu hii ya Sachangwan imekuwa kwa mazungumzo kila siku. Siku moja kufuatilia nyingine lazima kuwe na ripoti ya kwamba kuna ajali katika sehemu hii."
}