GET /api/v0.1/hansard/entries/771579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 771579,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/771579/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Tuwei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13436,
        "legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
        "slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
    },
    "content": "Asante sana, Naibu Spika wa Muda. Pia nami naunga mkono na kuwapongeza wale wote ambao tumewachagua siku ya leo kujiunga na viongozi wengine katika Bunge la Afrika Mashariki. Ni kweli kwamba hivi majuzi tulipokuwa katika Michezo ya Afrika Mashariki, tulipata kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki ilikuwa inangoja viongozi hawa wateuliwe na naona kwamba azma yao na matarajio yao yametimika siku ya leo. Nawapongeza watu wa Mosop na nawatakia kila la heri katika msimu huu wa Krismasi. Naomba madereva nchini waendeshe magari kwa njia iliyo safi ili tupate kuchunga usalama wetu katika barabara zetu. La mwisho ni kwamba nawatakia wenzangu Wabunge nafasi nzuri na kuwaombea dua tukutane Januari ili tuendeleze kazi nzuri. Nawatakia Wakenya umoja na mambo yote ambayo yanahusiana na umoja na ujenzi wa taifa letu yawe msingi wa kujenga nchi hii. Katika uchaguzi wa viongozi wa leo, vijana wawili wamechaguliwa. Hii imedhihirisha ya kwamba vijana wako na haki katika uongozi na wao wenyewe wanautafuta uongozi na kuupata. Wabunge leo wamedhihirisha ya kwamba chochote ambacho unakitaka utakipata ukitia bidii. Kwa hayo machache, Naibu Spika wa Muda, nakushukuru, nakupongeza na kukutakia kila la heri na wale wote ambao walikuteua kutoka pale Kibwezi."
}