GET /api/v0.1/hansard/entries/772944/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 772944,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/772944/?format=api",
"text_counter": 63,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Ahsante Mhe. Nderitu. Kwa hakika hiyo si shida ya maharaja kwa sababu ni shida ambayo ilijitokeza na watu wakakubali kwamba badala ya kutumia neno “halambe” tulitumie neno “harambe” kwa sababu linakubalika zaidi kwa watu kuliko halambe ambayo ilikuwa inakubalika kwa jamii ya waswahili peke yake. Kwa hivyo, hapo sina ugomvi wowote na Mhe. Nderitu. Bw. Spika, kwa wakati tulio nao sasa na shughuli za Bunge hili la sasa, kama walivyotangulia wenzangu kusema, itakuwa ni kuharibu wakati tukijadili maswala kama haya. Harambe iliyotumika hapa ni ya Kenya na si ya India. Tunajua harambe ya India ni tofauti na ya Kenya. Hivyo basi, tutoe kama siku saba ili aitwe mlalamishi na apewe fursa ya kujieleza mbele ya kamati husika, halafu maamuzi yatolewe. Lugha inakua kama alivyo sema mwenzangu mwengine na kila lugha ikuapo huomba sehemu tofauti tofauti. Kwa mfano, kwa Kiswahili nikisema “Sen. Kwamboka, makende” inatoa maana nyengine tofauti na kijaluo ambayo maana yake ni mpenzi wangu. Ahsante."
}