GET /api/v0.1/hansard/entries/773398/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 773398,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/773398/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 786,
        "legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
        "slug": "ruweida-mohamed-obo"
    },
    "content": ". Sikuja hapa kupendwa. Unaniambia umependa nini? Tuheshimiane. Nimetumwa hapa na kaunti ya Lamu. Namhurumia sana mama na watoto wa marubani wawili walioshikwa South Sudan. Hii siku ya leo watu wanafurahia Valentine’s Day ilhali wao wanahuzunika. Ningependa muda uongezwe. Waziri wa masuala za nje na wengine wafuatilie. Waharakishe ili wale marubani wawili walioshikwa kule na waasi baada ya ndege yao kuanguka waachiliwe huru. Marubani wamezuiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa. Nahurumia sana bibi yake na watoto, ambao hawana habari ni lini wataachiliwa. Ningependa pia kuwaeleza Mawaziri waharakishe kwa sababu watu wakisherehekea mambo mengine, nimesikia mwenzangu akisema watu huko Lamu wana huzuni. Wakazi katika miji ya Kizingitini, Bajumali, Chundwa na miji mingine wameambiwa kwamba nyumba zao zitavunjwa lakini hawakupewa ilani. Hawana raha. Hvi saa, sisi wakazi wa Lamu Mashariki tunataka hawa Mawaziri waangalie tatizo hilo. Tunataka maendeleo. Barabara yataka kujengwa lakini hiyo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}