GET /api/v0.1/hansard/entries/773800/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 773800,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/773800/?format=api",
    "text_counter": 192,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Asante sana Mhe Spika. Mimi pia nimesimama kuwaunga mkono hawa wenzetu ambao wameteuliwa katika nyadhifa mbalimbali. Kwanza ninakushukuru wewe na kamati ya uteuzi kwa kuwahoji hawa Mawaziri katika sehemu mbalimbali kuhakikisha kwamba wanachukua kazi zao katika ofisi zao. Ninawashukuru wanakamati kwa sababu nilikuwa nafuatilia wakiuliza maswali moja kwa moja kuhusiana na Mawaziri katika sehemu zao. Nilikuwa na furaha mno kwa sababu mlikuwa mnatuwakilisha sisi kama Wabunge. Kile nilifurahia mno ni kwamba mlikuwa mnawauliza mambo ya ufisadi katika nchi yetu ya Kenya. “Iwapo mtachukua ofisi zenu, kuhusu ufisadi mtasema vipi?” Tena kile nilifurahia ni nidhamu. Kuna wengi wanapewa ofisi. Hata tukiwa viongozi, hizo ofisi tunatakikana tuhudimie wananchi. Na wengine wakifika hapa na unaweza kujionea ndugu zetu kutoka mrengo wa NASA, wako hapa kungojea yale sisi tunatengeneza ili wafaidike. Ndiposa sisi kama viongozi tukisema nidhamu, ni lazima tuanze na sisi na hawa wameteuliwa katika nafasi hizi. Ninataka nimshukuru ndugu yangu kutoka upande wa magharibi. Sisi tulio mrengo wa Jubilee, wengi wamesema kwamba tulipeleka tumbo zetu katika chama hiki lakini hivi sasa, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}