GET /api/v0.1/hansard/entries/773801/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 773801,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/773801/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "kiranja wa Bunge hili ndugu Washiali anatoka upande wa magharibi. Spika katika Seneti anatoka upande wa magharibi. Hivi juzi, kamati ya uteuzi pia imechukua ndugu yetu Rashid kutoka upande wa magharibi. Iwapo watu wa magharibi wananiskia, wale wanaotoka Upinzani – na wako hapa sasa hivi, na wale walio nje – ninataka niwaambie kwamba sisi tumetunukiwa heshima na Rais pamoja na naibu wake kwa kutupatia nafasi katika Bunge hili na Mawaziri katika Kenya yetu. Nilikuwa nikifuatilia kuona Mawaziri watakaoteuliwa, na haswa akina mama. Mumemuona Dr. Monica Juma, ambaye alijibu maswali ana kwa ana na kueleza kazi ambayo amefanya katika nchi yetu ya Kenya, na hata katika zile sehemu ambazo amepewa. Mnaona kwamba alikuwa balozi. Amefanya kazi yake kulingana na taaluma yake. Sina wasiwasi kwamba amepewa hii nafasi kuwa kama Waziri wa mambo ya nje. Sina wasiwasi atakamilisha hiyo. Ukiona dada yetu Margaret, sina wasiwasi kwa sababu tunasema tunataka tusaidie akina mama na vijana wetu katika nchi yetu. Taaluma yake ilionyesha kwamba anaweza kufanya kazi yake vilivyo. Ndiposa ninasema nafasi ambazo akina mama wenzetu wamepewa zitawawezesha kuungwa mkono na akina mama wote nchini. Namshukuru dada yangu Sarah Korere kwa kuhakikisha kwamba amepigana na mwenzetu aliyekuwa anaitwa Lempurkel kupata nafasi hiyo katika Bunge hili. Nataka niwakumbushe sisi sote tuko sawa. Mimi huona wengine wanaongea kiingereza kingi sana lakini ukiwapatia kazi ya kufanya wanashindwa. Wengi hujigamba tu lakini wakipewa ofisi wanatumia ofisi zao vibaya. Pia, namshukuru dada yangu Farida kwa kupewa wizara ya ardhi. Hiyo imekuwa kizungumkuti katika nchi yetu ya Kenya. Katika sehemu za Trans Nzoia na magharibi mwa Kenya tuna shida ya mashamba. Shida hiyo inataka mtu ambaye anaifahamu kwa undani. Ndiposa namuunga mkono Rais kwa sababu wakisema kwamba wanataka kujenga kiwanda mahali fulani, matajiri hukimbia kununua shamba mahali hapo na kuwanyanyasa wenyeji. Ni kwa sababu wanajua faida watakayopata. Tutamuunga mkono dada yetu. Nauliza wenzangu wenye viti katika kamati wahakikishe kwamba wanamuunga mkono ili sera za mheshimiwa Rais ziweze kutekelezwa. Ninamshukuru tena ndugu yetu Munyes,ambaye siku moja alikuwa mwenyekiti katika chama cha FORD Kenya. Hakika, hakuwa na ubaguzi wa rangi au rika. Ninaamani kwamba katika wizara ya mafuta, ambayo ameteuliwa ashikilie, atatekeleza wajibu wake ipasavyo. Nilikuwa nakumbushwa na mwenzangu Lomenen na Joyce kuwa viongozi kutoka upande wa Lodwar wanachunga ardhi chini kwa chini. Maji na mafuta yako hapo. Tunajua na tunaimani kwamba Munyes atafanya kazi yake vilivyo. Nikimalizia ndiposa nipatie wenzangu nafasi, ninawashukuru wafanya kazi wa Bunge hili kwa sababu wamejitolea kinaga ubaga kuhakikisha kwamba wakipewa kazi katika kamati wanakosimamia wanaitekeleza vilivyo. Watu waache ofisi zao wazi ili sisi Wabunge tukitaka kuingia hapo, tukitaka kutatua matatizo ya watu wetu, hizo ofisi ziwe wazi na zihudumie wananchi wote wa Kenya; siyo wa kutoka kabila hili ama lile. Itatuwezesha pia tusonge mbele kama taifa. Asante kwa kunipa nafasi hii na asante kwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi."
}