GET /api/v0.1/hansard/entries/773818/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 773818,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/773818/?format=api",
"text_counter": 210,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Didmus Mutua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1885,
"legal_name": "Didmus Wekesa Barasa Mutua",
"slug": "didmus-wekesa-barasa-mutua"
},
"content": "Mhe. Spika, ukiangalia historia ya nchi ya Kenya, mipaka yake ilikuwa na usalama na imara zaidi wakati Waziri wa Mambo ya Usalama wa Nchi za Nje, Mhe. Njenga Karume, alikuwa kwenye usukani. Wapo wale wanaosema kuwa masomo ya Mhe. Njenga Karume alipata kwa kukaa na wasomi tofauti kwa sababu sio lazima uende shuleni ili upate masomo ama tajriba ya kuendesha mipango nyingi ya Serikali. Unaweza kukaa na daktari na uanze kufikiria kama daktari na pengine huenda ukapata ujuzi wake. Unaweza kukaa na mawakili na uwe na ujuzi wa kuelewa sheria za barabara na sheria zingine tofauti zilizoko katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo, ninaunga mkono hayo majina. Ningeomba wapewe nafasi ili waendeshe shughuli zao kama Mawaziri. Vile vile, ningependa kushukuru Kamati ya Uteuzi ambayo iliwapiga msasa. Ni Kamati ambayo ilikuwa na watu wenye tajriba tofauti. Wapo wale waliohusika na kutengeneza sera za Serikali ya Jubilee kwa nyanja tofauti na walikuwa wanawahoji wale kutaka kujua kama wanaelewa ama hawaelewi mipango ya Serikali. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}