GET /api/v0.1/hansard/entries/773819/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 773819,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/773819/?format=api",
"text_counter": 211,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Didmus Mutua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1885,
"legal_name": "Didmus Wekesa Barasa Mutua",
"slug": "didmus-wekesa-barasa-mutua"
},
"content": "Wapo Wakenya wengi sana ambao hivi sasa wanaishi na matumaini kwa kufuatia uteuzi wa Rashid Echesa Muhamed kwa sababu wanafikiria kwamba hata kama unatoka katika familia maskini ama isiyojiweza, familia ambayo wazazi wako hawajulikani angalau tu na chifu wa eneo lako ama mtaa ambao nyinyi mnatoka, unaweza kuwa Rais, Waziri wa nchi ama mtu ambaye utakuwa na umaarufu zaidi na kujenga jina hilo. Ningependa kuambia marafiki zangu wa mrengo wa Upinzani kuwa sasa hivi kuna mwamko mpya katika nchi ya Kenya kwa sababu vijana wale hawakuwa wanajulikana kwa jina wameweza kufika, hata wameweza kuwa Mawaziri. Wale watu ambao familia zao hazijulikani kabisa, kunaye mmoja ameweza kuwa Naibu wa Rais wa nchi ya Kenya kama Mhe. William Ruto. Ninafikiri, utuezi wa Rashid Echesa Muhamed umeleta mwanga unaoashiria kuwa Kenya lazima ijitayirishe. Mwaka wa 2022 tuwe tayari kuongozwa na Mkenya mwingine, kijana ambaye amekuwa akiuza mayai kwa jina la William Samoei Ruto kama Rais wa Kenya. Kwa hivi sasa, kila sehemu ya nchi ya Kenya inasubiri kuanza kuona utendakazi kwa hao wanawake na wanaume ambao wameteuliwa kama Mawaziri. Nasi kama Bunge lazima tuwape nafasi kwa sababu Rais anayeongoza Serikali katika nchi ya Kenya ni Uhuru Kenyatta. Yeye anajua nani anafaa kumsaidia ili atimize ndoto yake ama ahadi yake ambayo alipea Wakenya. Kwa hivyo ningependa ndugu zangu wa mrengo wa Upinzani, watulie."
}