GET /api/v0.1/hansard/entries/773820/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 773820,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/773820/?format=api",
"text_counter": 212,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Didmus Mutua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1885,
"legal_name": "Didmus Wekesa Barasa Mutua",
"slug": "didmus-wekesa-barasa-mutua"
},
"content": "Kuna wengi wa mrengo wa Upinzani ambao wake zao hawajafika hata kidato cha tatu ama darasa la nane lakini walilipa mahari na wanaishi sawasawa. Hata ukiangalia uongozi wa Upinzani wenyewe, utakuta kwamba Naibu wa Kiranja wa Bunge wa Chama cha Wachache, Mhe. Chris Wamalwa ni msomi maarufu maana alienda shule ya Havard na pia ako na uzamifu. Mkubwa wake kwa upande mwingine masomo yake nimeangalia hajafika darasa la tatu lakini yeye ni mkubwa. Kwa hivyo hao ndio walioanza mfano mzuri kwamba sio masomo ya darasa inayopeleka watu mbele bali ni masomo ambayo unajifundisha kila siku na hiyo ndio ya muhimu sana. Mhe. Spika, ninaunga mkono hii Hoja na ningependa kukomea hapo. Asante sana."
}