GET /api/v0.1/hansard/entries/77449/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 77449,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/77449/?format=api",
    "text_counter": 182,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Jambo la nidhamu, Bw. Spika. Majuma mawili yaliyopita, kulikuwa na Swali niliuliza Wizara ya Kilimo. Mawasiliano kutoka kwa wenyekiti wako, yalikuwa ni kwamba Waziri atafute jibu kabambe baada ya majuma mawili. Swali lenyewe lilikuwa linahusika na bei ya mahindi na vile vile, hatua za Serikali za kufungua ghala la halmashauri ya nafaka ili mahindi yanunuliwe kwa wakulima. Mpaka sasa hatujapata taarifa yoyote. Vile vile mawasiliano kutoka kwa kiti chako yalikuwa ni kwamba, Kamati ya Bunge inayohusika na ukulima ilichunguze hili swala na kutoa taarifa hapa Bungeni, kuelezea hatua ambazo Serikali itachukua ili wakulima wapunguziwe gharama ya kukaa na mahindi kwa sababu, hivi sasa, hakuna soko. Nilipitia kwenye shamba lako juzi na nikagundua kwamba pia wewe unahangaika kama mkulima yeyote yule, kwa sababu wamekosa soko la mahindi yao. Ningependa taarifa kutoka kwako."
}