GET /api/v0.1/hansard/entries/774676/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 774676,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/774676/?format=api",
"text_counter": 235,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "zimejaribu kurekebisha haya mambo na wanajitolea mhanga kusaidia. Mimi pia nitachukua jukumu huko kwetu na kuongea na gavana wangu ndio Lamu iwe kaunti ya sita kwa kusadia kurekebisha haya mabadiliko. Nimeshuhudia Mlima Kilimanjaro kutoka mwaka wa 2004 nilipoanza kazi. Nimekuwa nikipitia juu ya mlima huo nikiwa ndani ya ndege. Siku hizi, nikipitia hapo naona mabadiliko makubwa ya barafu iliyokuwa hapo awali na ile iko sasa. Nilisoma kwa kitabu kimoja kwamba barafu hiyo ikiyeyuka watu wa Lamu wanaathirika zaidi kwa sababu wanaishi baharini. Yale maji yanakuwa mengi na wanapata shida nyingi. Nimeona ni muhimu nichangie ili tuweze kuajibika pamoja. Huko Lamu kuna upande wa baharini na wa nchi kavu, kwa hivyo bahari ikijaa upande wa nchi kavu hupata changamoto nyingi kwa sababu ya haya mabadiliko. Wakati wa kiangazi kama sasa, kila mwaka Lamu tunaona vita vya wanyama wa porini na binadamu. Kwa sababu hiyo, tunazika watu ambao wameuwawa na viboko ama nyati. Baada ya mazishi huwa hawapati ile fidia kutoka kwa shirika la wanyama pori. Ni muhimu kama sisi sote tungeangazia hizi shida ambazo zinaletwa na mabadiliko haya. Nikimalizia, sehemu kama Lamu na zingine zina nishati za jua kwa masaa kumi na mawili kila siku. Kwa hivyo, ingekuwa muhimu kama jua lingetumika kutengeneza umeme ili tuache ile miradi ambayo inaleta athari kwa mazingira. Kwa sababu hii ni njia safi ya kusaidia kupunguza mabadiliko ya tabianchi. Asante."
}