GET /api/v0.1/hansard/entries/774685/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 774685,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/774685/?format=api",
"text_counter": 244,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia fursa hii nami pia niongeze sauti yangu kwenye suala hili la ruwaza ya Serikali Kuu kuhusu masuala ya mazingira na hasa hali ya anga na fedha za kuweza kufadhili masuala haya. Jambo la kwanza nitakalofanya ni kutoa shukrani kwa Waziri anayesimamia masuala ya kifedha ambaye ameona kuna umuhimu wa suala hili kujadiliwa sasa hivi. Si siri kuwa tumefanya masuala ya utani. Tumetania mazingira yetu. Hivyo basi Kenya hii imekuwa na matatizo. Mara kwa mara tukitoka kwenye hali ya ukame tunaingia kwenye hali ya mafuriko huku maji ya mafuriko yakimwagika na kuishia kwenye bahari Hindi bila kuwasaidia wananchi. Kama nilivyosema, masuala ya mazingira si utani. Hivyo basi Serikali Kuu katika hali ya kujadili suala hili imeona umuhimu kwa sababu masuala yale ambayo Serikali inataka kutekeleza yatakuwa hayawezekani. Kwanza, maji ndio uhai na bila maji hakuna pahali tunaweza kuendelea kwa sababu bila maji tutakuwa na shida ya kuwa na chakula cha kutosha kuweza kukidhi mahitaji yetu hapa nchini. Vile vile, tutakuwa na shida ya kuwa na ugonjwa kwa sababu hakuna maji ya kutosha. Si mchezo watu wanaona Afrika Kusini katika eneo la Cape Town watu wakipimiwa maji kwenye vibobo. Ni kuwa mazingira yale yameharibika na ukiangalia sana jambo lililowaleta pale ni masuala ambayo pia sisi tumeyatekeleza hapa tukiwa tunadharau mazingira. Mfano ni masuala ya kupanda miti inayokunywa maji kwa wingi. Suala hili nitalizungumzia nikimkumbuka mwendazake Waziri Mhe. Michuki ambaye alifanya kazi kwa muda mfupi kwenye wizara inayosimamia masuala ya mazingira na tayari tukaona tofauti kubwa sana. Jambo la kwanza alilofanya alisema kuwa miti yenye kunywa maji mengi yote iondolewe ili mito iweze kupata maji ya kutosha. Alivyoanza vile, tayari alianza kama mfano maeneo yao ya upande wa Kaunti ya Murang’a na vile vile kaunti nyingine jirani na kule anakoishi. Walivyoanza tu kukata ile miti kwa sababu ndiyo iliyokuwa inakunywa maji na kumaliza miti ili waweze kupanda miti inayofaa kutengeneza mazingira, basi mara moja kukaonekana tofauti kubwa sana. Nataka pia kumkumbuka mwendazake Profesa Wangari Maathai ambaye alifanya kazi kubwa sana ya kuhakikisha kuwa mito hapa nchini inapata maji ya kutosha. Ukipita maeneo na mazingira kule anakotoka utaona tofauti kubwa sana. Miaka kumi baada ya kupanda miti kulikuwa na tofauti kubwa sana. Hapa Nairobi, kuna hali ya uchafu na hali ya maji kupungua kwenye mto wa Nairobi. Vile vile Waziri mwendazake, Mhe Michuki, alifanya kazi na tukaona tofauti kubwa sana. Mto ulikuwa msafi na maji yakaongezeka kwa sababu ya kuzungumzia wananchi umuhimu wa kupanda miti. Nafikiria waziri mpya aliyekuja kusimamia masuala ya mazingira ana kazi kubwa sana ya kuhakikisha kuwa Wakenya wanawacha kutumia karatasi za plastiki ambazo zimekuwa zikitumika akiendeleza suala hilo kisheria kuwa kutumia karatasi zile ni makosa makubwa sana na ni kuvunja sheria. Vile vile, anapaswa kuhakikisha kuwa wananchi wanaambiwa umuhimu wa kupanda miti kwenye maeneo wanayotoka. Jambo la kwanza ni kuwa kama wazazi hawajajua umuhimu wa kupanda miti, basi watoto pia shuleni hawatajua umuhimu wa kupanda miti. Mara nyingi tumepeana miti kwenye shule na watoto wakadharau kwa sababu nyumbani kwao hawakulelewa kwenye maadili ya kuwa kuna umuhimu wa kupanda miti. Suala hili la pesa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}