GET /api/v0.1/hansard/entries/774686/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 774686,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/774686/?format=api",
    "text_counter": 245,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "za kuweza kusimamia masuala haya ni kitu ambacho si tu kiwe kimeandikwa kwenye vitabu vizuri vya Serikali bali kiweze kufuatilizwa na kuhakikisha kuwa pesa hizi zitatumika vilivyo. Mwanzo, Serikali yetu kupitia Waziri Keriako Tobiko ihakikishe kuwa suala la awali ni wananchi wapande miti. Kila mtu akipanda miti isiyopungua kumi kwenye mji wake tayari tutaona tofauti kubwa sana. Tumeharibu mazingira na tumeanza kuwa na shida ya maji. Hapa Kenya, mara nyingi hata maji yale ambayo yanakuja kwa wingi wakati wa mafuriko yamekuwa yakiishia chini, kupotelea na kufurisha bahari bure bila matumizi. Hivyo basi ndio Serikali iliamua kuwa bomba kubwa la maji litengenezwe ili lilete maji kutoka milimani upande huu wa Jimbo la Murang’a. Lakini mara nyingi, watu hawakulielewa suala lile. Ni maji ya mafuriko ndio yanaingia kwenye bomba lile ili maji yale yasiweze kupotea yaweze kutumika. Huku Kenya tumezoea kutegemea mvua ili itusaidie kupata chakula. Sasa hivi kuna umuhimu wa sisi kujua kuwa Serikali imetenga kando pesa za kuhakikisha kuwa tutanyunyizia maji mashamba yetu lakini juu ya kufanya hivyo, ni lazima pia sisi tuwajibike kuwa mashamba yetu yatumie si tu mvua peke yake bali maji yanayopatikana wakati wa mafuriko yakingwe ili yasaidie wananchi. Suala hili kama ninavyosema si utani. Ni suala ambalo limetukabili na litaweza kupigana na janga. Lakini, yote hayo tunayosema hayawezi kutendeka kama sisi kama wananchi na haswa sisi viongozi hatutachukua mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wananchi wanafuata ruwaza hii. Ruwaza hii isifuatwe tu kwa kungoja wakati pesa nyingi zitakuja bali tuanze mapema hapo awali tukitumia mifuko yetu ya Hazina ya Serikali Kuu ya Maendeleo ya Maeneo Bunge ili itusaidie wakati tunangojea masuala mengine yakitendwa na Serikali. Vile vile, tuanze kuzungumzia wananchi umuhimu wa sisi kutengeneza mazingira yetu. Mazingira yetu ndiyo yanayoweza kubadilisha hali ya anga ili tuwe na mazingira yanayofaa na anga inayofaa ili sisi kama Wakenya tuishi kwenye maeneo yanayotufaa. Pia nami naunga mkono ruwaza hii ya Serikali Kuu."
}