GET /api/v0.1/hansard/entries/775965/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 775965,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/775965/?format=api",
"text_counter": 224,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Obo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 786,
"legal_name": "Ruweida Mohamed Obo",
"slug": "ruweida-mohamed-obo"
},
"content": "Asante Bwana Spika. Ninashukuru umenipatia nafasi hii nami niweze kuchangia hii sera ya makazi. Kwa ruhusa yako, naomba nisome jinsi Katiba inavyosema kwa lugha ya Kiingereza. The Constitution states that every person has a right to access adequate housing and a reasonable standard of sanitation. Further, Article 21(2) states: “The State shall take legislative, policy and other measures including the setting of standards, to achieve the progress realisation of the rights guaranteed under Article 43.” Hii Sera ni muhimu sana. Saa hii katika Eneo Bunge la Lamu Mashariki kuna barabara inayojengwa. Barabara hiyo inatoka Mtangawanda ikielekea Kizingitini. Ni maendeleo mazuri ambayo tunafurahia. Lakini Katiba inasema kuwa watu wawe na nyumba. Kule, nyumba zinavunjwa. Sio kwamba nyumba zimefuata barabara ila barabara ndio imefuata nyumba. Pia, nyumba hizo zimechorwa alama ya “X”. Watu wametishika sana hata bodaboda ikipita wanaona ni kama trakta inakuja kuvunja nyumba. Ni muhimu sana sera hii ipitishwe kusikuwe na unyanyasaji wa watu na kuwe na haki za kibinadamu. Kama saa hii, inasemekana kuwa ni minazi peke yake ndio italipwa Kshs3000 kwa kila mnazi. Ardhi haihesabiwi. Wakikata mwembe, mkwaju au mkorosho, hazihesabiwi. Watu wananyanyaswa sana. Serikali inafanya bidii kuleta miradi na sisi tunaipenda lakini wale wanaokwenda kule mashinani ndio wanatuharibia. Wanatufanya sisi Wabunge wa Lamu kupata shida. Watu wanaona sisi pia tuko kwa Serikali na tunachangia mambo haya. Ukizungumza kuhusu vile ambavyo kontrakta na wahandisi wanafanya unaonekana pengine unapinga miradi ya Serikali. Sisi watu wa Lamu hatupingi miradi ya Serikali. Tumeshirikiana kama Wabunge kuwasaidia wananchi ndio maana nikaona leo niwaeleze kuwa hii sera ilikuwa ipitishwe mwaka mmoja kabla ndio haya mambo yanayotokea Lamu yasitokee. Sisi watu wa Lamu twapenda sana miradi lakini twataka iangaliwe kwamba wale wanaokuja kule ndio wanaharibia Serikali. Hii ndio maana huko Lamu kila wakati watu wanasema tuko marginalised, tumetengwa, tumefanywa hivi na husababisha hasira na watu wengine kuona mambo mengine mabaya. Naomba wale wahusika kuwa kabla sera hii haijapita wahakikishe hizo alama za “X” walizochora wazifute. Tukiziona hizo alama za “X” tunajua watazivunja. Basi wahakikishe wamezifuta ama watafute njia ya kuwasaidia wananchi wa Lamu ili tujihisi tuko ndani ya Serikali. Hivyo, tutakaribisha miradi kwa njia nzuri. Ahsante."
}