GET /api/v0.1/hansard/entries/776014/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776014,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776014/?format=api",
"text_counter": 273,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Asante Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii inayohusiana na maswala ya usalama katika nchi yetu hususan katika sehemu ya Wajir. Kwa kweli, swala la usalama ni swala nyeti sana. Limeweza kushuhudiwa mara kadhaa na limeweza kuleta madhara katika sehemu nyingi. Pia, limeweza kuleta madhara katika uchumi wetu, elimu ya watoto wetu na afya ya Wakenya. Si mara ya kwanza swala hili kujadiliwa Bungeni katika swala zima la usalama. Kule kutokana kwa mara kadhaa Bungeni inamaanisha kwamba limekuwa ni donda sugu. Kwa maana hii, linaonekana kwamba haijapatikana suluhisho katika swala zima. Ingawaje ningependa kushukuru Serikali kwa juhudi zake katika swala hili zima la usalama katika sehemu nyingi ambapo pameshuhudia matatizo kama hayo, swala la usalama halipaswi kuangazia yale ambayo tunayafikiria hivi sasa kwamba kuna kikundi cha Al Shabaab kinachosababisha kutokuwa na usalama hapa nchini. Swala hili ni swala nyeti na kisha ni swala ambalo ni lazima tuliangalie kwa pande zote. Kutokuwa na usalama katika nchi yetu mara nyingi ni sisi Wakenya ama viongozi tunaosababisha hali hii ya kutokuwa na usalama. Utapata kuwa Serikali inatumia The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}