GET /api/v0.1/hansard/entries/776015/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776015,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776015/?format=api",
"text_counter": 274,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "rasilmali zake na nguvu nyingi kupambana na mambo ambayo hayastahili. Utapata majeshi yetu na walinda usalama wetu wanapelekwa katika sehemu nyingine kupambana na wananchi wa kawaida. Yote haya ni mifano mibaya katika nchi yetu na nchi za nje. Kwa hivyo, tunapojadili swala hili na kuliangalia, ni lazima tuangalie pande zote katika hili swala zima ili tupate suluhisho juu ya maswala kama haya. Ikiwa sisi wenyewe kama nchi ndio mara nyingine tunasababisha matatizo haya, je yule mwingine ambaye ni adui atafanya nini? Naibu Spika wa Muda, kwa kweli adhari ni nyingi kama nilivyosema hususan nikuzungumzia maswala ya Eneo Bunge ninalotoka ama kaunti yangu ya Lamu. Hivi sasa, wazazi wameshindwa kupeleka watoto wao shuleni ijapokuwa Serikali imefanya kusoma ni bure. Lakini kwa sababu uchumi umefifia, na uchumi mkubwa wa kaunti ya Lamu ni watalii, utashangazwa hivi sasa kuwa uchumi wa utalii ndani ya Lamu Kaunti umefifia kwa asilimia 80. Hivyo basi kusababisha uchumi kufifia katika eneo hilo na kusababisha yale matatizo ya kiuchumi katika sehemu hiyo. Ni vyema lifahamike pakubwa kwamba hakuna maisha yanaweza kuendelea katika nchi hii ikiwa viongozi na Serikali haitokaa kidete kulitatua swala hili. Hakuna maendeleo yoyote wala uchumi utakaokua. Naibu Spika wa Muda, kwa masikitiko makubwa kutokana na hayo kama nilivyosema, sisi tukiwa viongozi tunajaribu kuchochea hayo. Kwa mfano, ni masikitiko kuona kwamba kiongozi mwenzangu kutoka Lamu amezungumza kuwa kuna nyumba zinavunjwa na kadhalika. Nataka kuhakikishia watu wa Lamu kuwa hakuna kitengo cha usalama hata kimoja kimepewa ilani ya nyumba yoyote kuvunjwa kwa sababu ya maendeleo ya barabara. Lakini lugha kama hizi zikiletwa hapa Bungeni zinatia watu hofu isiyokuwa na maana. Hakuna nyumba inayovunjwa na hakuna ilani yoyote imetoka kwa Serikali kuvunja hizo nyumba."
}