GET /api/v0.1/hansard/entries/776057/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 776057,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776057/?format=api",
    "text_counter": 316,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady Bady Twalib",
    "speaker_title": "The Member for Jomvu",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo imeletwa na ndugu yetu, Mhe. Rashid Kassim. Kwanza, nataka na mimi nifanye kama vile dadangu Janet alivyowashukuru watu wa kwake. Na mimi ninataka kuwashukuru wananchi wa Eneo Bunge langu la Jomvu kwa kunichagua kwa mara ya pili niwawakilishe katika Bunge hili. Walinichagua mwaka wa 2013 nikiwa kijana mwepesi na wakanichagua mwaka 2017 nikiwa Garang De Mabior – mzee fulangenge. Kwa hivyo, nawashukuru sana wananchi wangu wa Jomvu. Vile vile, natoa rambirambi zangu kwa niaba ya wananchi wa Jomvu na mimi mwenyewe kwa watu wa Wajir kwa vile walipoteza maisha. Nasema jambo kama hili si jambo ambalo linafaa kuvumiliwa katika nchi ya Kenya. Naisihi Serikali hii yetu ifanye juhudi zaidi kwa wale wananchi wa kule. Kitu muhimu ambacho mimi nakubaliana nacho ni kuwa wananchi katika sehemu ya Wajir hawataki hata mara moja kupoteza maisha yao. Kwa maana hiyo twasema wanajeshi wetu wanaofanya kazi katika sehemu ya Mogadishu na sehemu nyingine katika nchi ya Somalia wahakikishe kuwa wanakuja katika mipaka yetu ili waonekane kwamba wanafanya kazi, na interest ya wananchi wetu wa Kenya ndio ya kwanza kuliko mtu mwengine yeyote. Jambo la muhimu ambalo nataka kulisema leo ni kuwa jeshi letu la Kenya ni lazima lidhibiti kisawasawa mpaka wa Somalia na nchi yetu ili wananchi waishi kwa njia nzuri. Uhalifu haujui dini wala kabila. Kwa maana hiyo, wale ambao watakuwa wanazungumzia mambo ya ugaidi kama mambo yanayohusiana na dini ya Kiislamu ni jambo la uongo na ambalo halipo katika fikra kwa sababu dini yetu hairuhusu mtu yeyote yule kufanya makosa kwa mwanadamu mwengine yeyote. Dini inahimiza usimfanyie mtu jambo ambalo wewe mwenyewe hutaki kufanyiwa. Kwa hivyo, hawa ni watu ambao wanafanya uhalifu na ni muhimu wachukuliwe kama wahalifu wa kawaida ambao nchi lazima ijithibiti kuona namna watu hawa watashikwa ili watu wa sehemu mbalimbali kama vile Wajir waweze kuendelea na maisha yao. Tunaona kuwa hao ni walimu ambao walikuwa wakitoa msaada mkubwa kwa sababu elimu ndio chombo kikubwa sana kwa maisha. Tunafaa tuikemee sana hali kama hii ya kuwalenga walimu na tutaungana mkono na ndugu yetu Mhe. Rashid Kassim. Mimi Mbunge wa Jomvu ambaye nimesimama hapa nampongeza kwa sababu ni mwezi uliopita tu tulikuwa Wajir The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}