GET /api/v0.1/hansard/entries/776662/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776662,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776662/?format=api",
"text_counter": 285,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Asante Mhe. Spika wa Muda. Ningependa kuungana na wenzangu kumpongeza Mwenyekiti wa Kamati hii pamoja na kamati yake kwa kazi nzuri ambayo wameifanya. Tunalolizungumzia leo hapa ni Mswada muhimu sana katika nchi yetu. Unahusiana na barabara zetu, mipangilio ya Serikali na utaratibu wa kuinua hali ya barabara zetu nzuri. Kitu muhimu ambacho nataka tufahamu kwanza ni kujua umuhimu wa barabara katika nchi yetu na katika ulimwengu kwa ujumla. Vile vile, nataka tufahamu katika nchi yetu ya Kenya ni hatua gani tumepiga katika suala nzima la barabara. Kwa kweli, mbali kwamba tutaipongeza Serikali ilioko kwa juhudi zake bado kuna matatizo ambayo yako. Kuna malalamiko kutoka kwa Wakenya, ambapo naamini pakubwa Serikali inajitahidi ili kuweza kulifanikisha jambo hili. Lakini kwa upande mwingine kuna matatizo ambayo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}