GET /api/v0.1/hansard/entries/776663/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 776663,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776663/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "yanaonekana kupitia kwa wanakandarasi wanaopewa kandarasi hizi ama kupitia wale wahusika wanaopewa kuendesha jambo hili. Mhe. Naibu Spika wa Muda, utakubaliana nami kwamba barabara ni muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya kwa sababu inarahisisha usafiri na vile vile inainua uchumi wa sehemu yoyote ambayo kuna barabara nzuri. Tutaweza kufaidi vipi mambo kama haya katika hili suala nzima? Tatizo liko Serikalini au wahusika vile nilivyosema? Tatizo liko kwa wahusika na kandarasi. Mhe. Naibu Spika wa Muda, Serikali inatumia pesa nyingi sana katika sekta hii ya barabara. Bilioni za pesa zinatumika kila mwaka tunapopanga Bajeti ya nchi. Mbali kwamba bilioni za pesa zinatumika, suala hili linaonekana bado lina tatizo na Wakenya na viongozi wenzangu wameweza…Kwa masikitiko makubwa, tunapozungumza, kuna baadhi ya maeneo Bunge ambayo hayana hata kilomita moja ya barabara ya lami tangu tupate Uhuru. Hata zile sehemu ambazo barabara zipo, utapata zimejengwa kwa hali duni kabisa. Kwa mfano, unaendesha gari kwa masaa matatu ama manne ilhali ni sehemu unaweza kutumia dakika kumi au ishirini kufika. Haya yote yamesababishwa na kutoajibika kwa wahusika waliopewa majukumu haya. Ni lazima tuyazungumze ili yafahamike kwa sababu ikiwa ni kosa lilifanyika jana, hatutaki lifanyike tena kesho. Ni lazima kupatikane ushirikiano. Suala hapa sio la kujenga barabara pekee bali ni kuzingatia masharti yote kwa sababu ya siku zijazo. Nchi yetu inapanuka, idadi ya watu inaongezeka na magari yanaongezeka lakini leo utapata mipangilio inayofanywa kujenge barabara si sawa. Utapata kwamba baada ya miaka mitano au sita barabara hazina nafasi tena ya kupanuka. Waliopanga kutengeneza barabara zile hawakuweza kufikiria mambo kama hayo. Hayo ndiyo matatizo tumekuwa nayo. Serikali za kaunti zimepewa majukumu ya kusawazisha mambo hayo na ni jambo nzuri. Hatuangali suala la kaunti, Mbunge ama pengine KeNHA, KURA na kadhalika bali tunachoangazia ni uajibikaji wa hao wote ambao watapewa majukumu ya kutengeneza barabara hizi. Huku tukiendelea kujadili Mswada huu, ninaomba tuupitishe katika Bunge hili ili mipangilio ya kuzijenga babara hizi uendelee. La msingi ni kwamba Serikali yoyote itakayochukua usukani ihakikishe kwamba miundo msingi na matekelezo yametekelezwa kisawasawa na wahusika wakuu wameweza kuwajibika katika hili suala nzima. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa masikitiko makubwa, utapata barabara imejengwa kutumia bilioni za pesa lakini haidumu hata miaka miwili kabla Serikali tena kutumia pesa zingine kuikarabati. Kutokana na tatizo hili, ningependa kutoa maoni yangu katika suala hili nzima. Ikiwa mwanakandarasi amepewa kazi ya kutengeneza barabara, ni vyema kuwe na mkataba baina ya mwanakandarasi na Serikali ya kuhakikisha kwamba kwa muda wa miaka mitano au kumi, kwa gharama ile ile aliyopewa kutengeneza barabara, atahakikisha aimekarabati bila Serikali kutimia pesa zingine. Kwa nini Serikali itumie kati ya Ksh2 bilioni hadi Ksh10 bilioni kumpea kandarasi ya kutengeneza barabara kisha baada ya miaka miwili, Serikali itafute pesa kwenda kuifanyia marekebisho barabara hiyo hiyo? Kwa hivyo, ili pesa hizo ziweze kuwasaidia Wakenya kwa namna nyingine, ningependa Serikali ihakikishe kwamba mwanakandarasi huyo ameingalia barabara hiyo kwa muda wa miaka 10. Ikiwa kutakuwa na tatizo, yeye ndiye atahusika kwenda kuirekebisha barabara ile."
}