GET /api/v0.1/hansard/entries/776667/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 776667,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776667/?format=api",
    "text_counter": 290,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ali Sharif",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Nataka kuipongeza Serikali kwa juhudi zake nikizungumzia Eneo Bunge la Lamu Mashariki na Kaunti ya Lamu kwa jumla. Kwa mara ya kwanza, wakazi katika Kaunti ya Lamu wameweza kupata barabara ya lami. Lakini kwa masikitiko makubwa, mwanakandarasi anayetengeneza barabara kutoka Garsen mpaka Lamu ana mwaka mmoja hivi sasa ameshapewa cheti. Mheshimiwa Rais ametia barabara wakfu lakini mwanakandarasi huyo hajatengeneza barabara hiyo, na haya ndiyo matatizo. Tuko na barabara ambayo inatoka Lamu kwenda Kiunga. Tunasikia mara kwa mara kuna magaidi na kadhalika. Barabara hiyo ikitengenezwa na iwekwe lami, itasaidia pakubwa katika masuala haya. Kwa hivyo, mimi naunga mkono lakini kama nilivyosema, tukiwa kama viongozi, twataka tuyajadili vizuri masuala haya na tuhakikishe tumeyaweka sawa kwa sababu ya siku zijazo. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}