GET /api/v0.1/hansard/entries/776669/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 776669,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776669/?format=api",
    "text_counter": 292,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili mimi pia niweze kuchangia Mswada huu. Ningependa kuunga mkono Mswada huu kwa sababu una mambo mengi mazuri kuhusu miundo msingi katika nchi yetu ya Kenya. Pili, ningependa kumshukuru Mwenyekiti wa kamati ya barabara, Mhe. Pkosing, ambaye namjua vizuri kwa utendakazi wake. Ni mheshimiwa ambaye tulifanya naye kazi katika Bunge ambalo lilipita na katika Bunge hili leo twafurahi kuwa tuko pamoja naye katika mambo haya ya barabara. Vile vile, ningependa kumtambua Mhe. Maina Kamanda ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Barabara wakati wa nyuma. Binafsi, katika Bunge la Kumi na Moja, katika sehemu yangu ya uwakilishi kulikuwa na barabara ambayo ilikuwa inaitwa Hakika, mahali panapoitwa Madafuni. Barabara hiyo ina msongamano mkubwa sana wa magari ya kutoka Nairobi kuingia Mombasa. Eneo Bunge langu la Jomvu ndilo linakaribisha watu katika jiji la Mombasa. Ujenzi wa barabara hiyo ulipewa mwanakandarasi, Blue Chips Ltd., ambaye alisumbua watu sana kwa muda wa karibu miaka saba. Lakini tukishirikiana na Mhe. Maina Kamanda - alinisaidia akiwa mwenyeketi wa kamati ya Bunge kuhusu barabara - leo hii barabara imetengenezwa na iko katika hali nzuri."
}