GET /api/v0.1/hansard/entries/776675/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776675,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776675/?format=api",
"text_counter": 298,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Kipengele cha 96 chazungumzia habari. Kuna shida kubwa hapo. Kwa hivyo naunga mkono Mswada huu zaidi. Nikipeana mfano, watu wa KURA wanataka kutengeneza barabara kwangu lakini wanasema eti wananchi wakae chini wajadiliane kisha ndiyo wapeleke maafikianao kwao. Ndiposa nilisema si sawa hivyo. Wao wanataka kutengeneza barabara. Kwa hiyo waje wazungumze na wananchi huko mashinani na kusema wanataka kujenga barabara fulani kwa ajili ya jambo Fulani. Kwa hivyo, mimi nikiungalia Mswada huu naona una mambo mengi mazuri. Siku chache zilizopita Mhe. Rais Uhuru Kenyatta alikuja Shika Adabu kule Mombasa. Nilisimama na kusema hatuwezi kupanua bandari yetu ya Mombasa bila kupanua externalinfrastructure . Barabara ni lazima zipanuliwe. Kwa maana hiyo mimi nashukuru kwa sababu barabara hivi sasa zinapanuliwa kutoka Mlango wa Kenya Ports Authority (KPA) kupitia kwenye eneo bunge langu. Mswada huu unasema kwamba ikiwa kuna kitu chochote ambacho unahitaji kirekebishwe ni lazima utoe notisi ya miezi sita. Ni kweli Wachina wako pale kwangu wakitengeneza barabara nzuri lakini hawakutoa notisi ya kutoa mifereji ya maji katika sehemu ya Mikindani. Leo hii panapotengenezwa barabara kule kwangu wakazi hawana maji. Sheria inawahitaji wajenzi wa barabara watoe notisi ya miezi sita kwa Mombasa Water and Sewerage Company ambao husambaza maji ili wapate nafasi ya kutoa mifereji yao na kuiweka mahali pengine. Leo hii kwa sababu barabara inatengenezwa ndani ya eneo bunge langu, sehemu ya Mikindani, wananchi hawana maji kabisa. Ukiangalia ndani ya Miritini watu hawana maji kwa sababu pipe zimeharibiwa na barabara. Hata ndani ya sehemu ya Jomvu Kuu pia watu hawana maji kwa sababu sheria haikufuatwa. Mwenyekiti wa Kamati inayosimamia barabara, ambaye ni rafiki yangu, yuko hapa. Tafadhali tushikane mikono tuangalie jinsi tutakavyoweza kuthibiti tatizo hili ili wananchi wasifurahie barabara huku wanakufa kwa kiu. Tuangalie kuwa mambo haya yanaenda sambamba. Barabara itengenezwe na watu wapate maji ili wafurahie mradi ambao umeletwa kwao kuwa umeletwa kwa njia ya manufaa. Yote tisa lakini mimi kama Mbunge nimefurahishwa na barabara ambayo inatoka Kilindini na ambayo itakuwa dual carriageway ya kupita katika sehemu yangu. Barabara ile ikimalizika msongamano mkubwa wa magari ambao ulikuwa ukishuhudiwa katika magari ya kutoka Nairobi na kwenda mpaka Mombasa utaisha. Mhe. Naibu Spika wa Muda, nakumbuka ni mwaka juzi tu ulipotoka Mombasa. Wewe ni rafiki yangu. Ulitaka kwenda moja kwa moja mpaka Mtito Andei lakini ulikwama kwa barabara katika sehemu ya Miritini mpaka ukanipigia simu ikabidi nimuite OCPD aje akufungulie barabara ili uweze kupita uende sehemu yako ya Mtito Andei. Kwa hivyo hili ni jambo ambalo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}