GET /api/v0.1/hansard/entries/776676/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776676,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776676/?format=api",
"text_counter": 299,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "hatutaki tena litoke katika nchi inayokua kama Kenya. Tunataka tuone barabara zetu zimenawiri na kuwa sawasawa. Kama Mbunge mwenzangu alivyozungumza hapa, barabara ya kutoka bandarini ambayo inaitwa gateway to East and Central Africa ndiyo barabara ambayo inafanya biashara katika nchi zetu za Uganda, Rwanda, Burundi na sehemu nyingine kunawiri. Kwa hivyo, ni lazima barabara hizi zitengenezwe na namwambia mwenyekiti wa Kamati inayosimamia barabara kwamba tutashirikiana pamoja na Kamati yake katika sehemu zetu tofauti ili tuweze kukuletea matatizo yetu tuone kuwa tumeyatatua kwa ajili ya wananchi wetu ambao wametuchagua. Kwa hayo machache, nakushukuru Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii ili nizungumze na kuchangia katika Mswada huu wa barabara. Asante na Mwenyezi Mungu akubariki."
}