GET /api/v0.1/hansard/entries/776918/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776918,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776918/?format=api",
"text_counter": 201,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Kwanza ningependa kutoa kongole zangu kwa wale ambao wameweza kuchaguliwa katika taasisi hii ya Bunge. Taasisi hii ni kiungo muhimu sana kwa Seneti na hata Bunge la Kitaifa. Kwa hivyo, nawaunga mkono wote walioweza kuchaguliwa. Wale waliopendekezwa ni watu ambao nimeweza kufanya kazi kwa karibu sana, kwa mfano ndugu yangu, Sen. George Khaniri, ambaye anafanya mazungumzo upande ule na mdogo wangu, Sen. Aaron. Sen. George Khaniri ni mwalimu wa sheria za hapa Bungeni. Kwa hivyo, najua kwamba atapeleka akili hiyo katika taasisi hii ya bunge. Vile vile mdogo wangu, ambaye naelewana naye sana, Sen. Aaron, ana uwezo, nguvu, akili na maarifa ya kuweza kuendesha kazi katika taasisi hii ya Bunge. Vile vile, Sen. Beth ni dada ambaye namheshimu sana. Ni mkakamavu sana katika upande wa siasa. Najua kwamba alitekeleza jukumu hili hapo awali na ataendelea kulifanya. Nakutakia kila la heri, dada yangu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}