GET /api/v0.1/hansard/entries/776920/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776920,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776920/?format=api",
"text_counter": 203,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "La muhimu ni kuona ya kwamba kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili mheshimiwa wetu mmoja kutoka eneo la Pwani, haswa zaidi Kilifi, dada yetu Mhe. Aisha Jumwa, ameweza kupendekezwa kuhudumu katika taasisi hii ya Bunge. Hii inafanyika kwa mara ya kwanza kuanzia mwaka wa 1963. Tuna imani kwamba Mhe. Aisha atatekeleza jukumu hili vizuri. Bw. Spika, hata hivyo ningependa kusema kwamba sio kila kitu kinaenda sawa katika tume hii ya Bunge. Kuna mambo fulani ambayo tume inayoondoka haikufanya. Kwa mfano malipo ya mileage iliondolewa, ingawa tumesikia ya kwamba huenda yakarejeshwa. Vitu vingine vilikuwa vimeondolewa. Kwa hiyo, wale ambao tunawachagua hivi sasa wanafaa kututetea zaidi. Wa muhimu zaidi pia ni wafanyakazi wa hapa ndani ya Bunge. Sisi kama viongozi tunapata lawama. Tunambiwa mambo kadhaa kuwahusu wafanyakazi. Kama alivyosema Kiongozi wa Wengi, Sen. Murkomen, hawa wafanyakazi wanafanya kazi ngumu sana. Kwa mfano, Mbunge akiongea kitu ambacho hakifai, Bw spika husema atolewe nje. Kumtoa mbunge ndani ya Bunge sio rahisi hivyo. Kwa hiyo wafanyakazi wa Bunge wakikufuata na kukuambia utoke, utatoka. Kwa hivyo, kazi zao ni ngumu sana, hasa kuhakikisha kwamba hakuna upande unaopendelewa. Kwa muda wote ambao wamekuwa wakifanya kazi hapa ndani ya Bunge, maafisa wetu wa Serjeant-At-Arms hawana muungano wa kutetea haki zao au trade union. Maafisa wa Serjeant-At-Arms na wale wa Hansard wamekuwa wakijipata katika hali ya sintofahamu. Wafanyakazi wengine wa Bunge wako na directorates lakini wale watu wa"
}