GET /api/v0.1/hansard/entries/776922/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776922,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776922/?format=api",
"text_counter": 205,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "na Hansard hawana directorates . We will let them to manage their ownaffairs because they know themselves better. They know who is competent and who is not. Wao wenyewe watajua la kufanya. Bw. Spika, kuhusu swala la kupandishwa vyeo na kuajiriwa kazi kwa watu kutoka maeneo tofauti tofauti ya Jamhuri yetu ya Kenya, siwezi kusema mengi. Hii ni kwa sababu nimekuwa na ufahamu mwingi kwa muda nimekuwa hapa. Nimekuwa katika Bunge la Kumi na Moja na sasa katika Bunge hili la Kumi na Mbili. Ni maoni yangu kuwa tunapogawa nafasi za kazi, tuhakikishe kuwa makabila yote 43 yanaakilishwa katika tume ya Bunge letu la Kenya. Wakati huu, mambo sivyo. Hapa tuna Sen. Aaron Cheruiyot, Sen. George Khaniri, dada yangu, Sen. Beth Mugo, Mhe. Aisha Jumwa na wengine ambao sina uzoefu wa karibu nao. Itakuwa vyema kwao ikiwa wakati wa kuaajiri wafanyakazi hapa Bungeni watahakikisha taifa nzima limeakilishwa. Kazi yao itakuwa rahisi wakifanya hivyo. Mwisho ni kwamba, pesa za Seneti na pesa za Bunge la Kitaifa zimekuwa zikitofautiana. Ni wajibu wao waliopendekezwa hapa kuona ya kwamba tofauti hizi zimepungua kwa sababu sisi sote tuko sawa. Pesa zetu ambazo zinapelekwa katika Bunge la Kitaifa, hazifai kubadilishwa kwa senti moja. ."
}