GET /api/v0.1/hansard/entries/776935/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 776935,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776935/?format=api",
"text_counter": 218,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Gona",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13176,
"legal_name": "Christine Zawadi Gona",
"slug": "christine-zawadi-gona"
},
"content": "Asante Bw. Spika kwa nafasi hii. Naunga mkono tume iliyoteuliwa na ninafurahi kwamba kwa mara ya kwanza sisi pia tumezawadiwa. Ni kama kila siku unaenda shuleni kuzawadi watoto wa wengine lakini mtoto wako hafanyi vizuri. Nina furaha kwa sababu ya majina yaliyoletwa hapa, hasa jina la Mheshimiwa Beth Mugo. Yeye na mimi tuliteuliwa. Kuna shida nyingi sana ambazo wabunge walioteuliwa hupitia katika mabunge haya. Mara nyingi tunaonekana kama hatustahili ama tulikuja hapa kwa bahati mbaya. Mimi kama Seneta si tofauti na mwenzangu aliyechaguliwa kwa sababu majukumu ni yale yale na shida ninazopata ni zile zile. Mwananchi wa kawaida hajui kwamba mimi niliteuliwa ama nilichaguliwa. Yeye anajua kwamba mimi ni Seneta. Mimi pia hupata jumbe za kutafutia watu kazi na mambo mengine. Ninamsihi Mheshimiwa Beth Mugo, kwa vile yeye ndiye tunayemtegemea, ahakikishe sisi wenzake hatuteseki. Nimesikia kwamba kuna pesa za kwenda mashinani kuhakikisha pesa zinazopelekwa kule zinatumika vizuri. Nasikia fununu kwamba sisi pia tutapewa pesa hizo. Kwa hivyo namsihi awe mstari wa mbele kututetea ili sote tupate. Nashukuru pia kwa sababu kuna wanawake watatu na hivyo si vibaya. Zaidi ya hayo, kuna wafanyakazi ambao wataandikwa. Wakati watakakuwa wakifanya hivyo pia waangalie kina mama wenzetu. Bunge linafaa kuwa na sura ya Kenya. Shinda The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}