GET /api/v0.1/hansard/entries/776954/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 776954,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/776954/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wa mambo ya Bunge na pia Sen. Khaniri ambaye amehudumu katika Bunge kwa muda mrefu. Jambo ambalo ningependa kuwasisitizia n ikwamba tumewapa fursa hii kututumikia sisi, maseneta na wabunge. Sio kwamba wanaujuzi zaidi au wao ni bora kutuliko, ila tumewapa fursa hii kututumikia kwa sababu ni dhamana ambayo tumewapa kuhakikisha kwamba masilahi ya wabunge na masilahi ya maseneta yanaangaliwa kikamilifu wakati tunahudumu katika Bunge hili. Tumeshuhudia kudhorora kwa huduma zinazopewa wabunge kama vile mileage, na hata huduma za dining zimedhorora. Ninatumaini kwamba Tume hii ambayo tumechagua leo itaingilia mambo haya na kuona kwamba yote yanafanywa kwa njia sawa sawa. Kazi ya Seneta sio kazi rahisi. Juzi tulimuona Sen. (Prof.) Kindiki akishuka kwenye chopper yake, alivua nguo na akaingia kujenga nursery school kwa niaba ya watu wake wa Tharaka Nithi. Kazi ya Seneta sio rahisi bali ni kazi ngumu. Kuna wakati unahitajika kuingia mitaani kufanya kazi ambayo hungeweza kufanya kama ungekuwa umebaki katika zile profession zetu. Mimi ni wakili kama Sen. (Prof.) Kindiki. Haingekuwa rahisi kwangu mimi ama Sen. (Prof.) Kindiki kuingia mahali na kuvua shati, kukunja suruali ndefu ili akanyage udongo ndiposa atandike nyumba kujenga shule kwa watu wake. Kwa hivyo, ni lazima tupate mishahara ya kisawa sawa na pia tupate mileage na mengine ambayo wenzangu wameweza kuyazungumzia wakati walikuwa wakichangia. Jambo ambalo ningependa kusahihisha ni kwamba Mhe. Shabaan pia nimjumbe anaye toka sehemu za pwani. Kwa hivyo, wale walitangulia kusema kwamba ni mara ya kwanza mtu wapwani kupata fursa hii, sio hivyo. Mhe. Shabaan pia anatoka pwani lakini kwa sasa, tumepata mtu kutoka ile pwani ya chini. Kuna pwani ya juu upande wa Taita na Kwale, lakini sasa tumepata pwani ya chini ambayo ni bora zaidi karibu na ndugu zetu wa Lamu kwa akina Mhe. Loitiptip. Vile vile, tungependa wafanyikazi wahii Tume ya bunge wawe na sura ya Kenya na sio sura ya mahali pamoja. Inafaa kuwe pia na Waturkana ndiposa Seneta wa Turkana aweze kuzungumza nao ili ajue habari za kwao. Wamaasai pia wanafaa kuwepo. Inafaa kuwe n amtu mmoja au wawili kutoka Elgeyo-Marakwet kule kwa Sen. Murkomen na hata wakutoka Lamu ambaye atatayarisha chai ya saa kumi na mahamri na mambo kama hayo. Kwa hivyo, hatungependa Tume hii iajiri watu kutoka katika kaunti ya Nairobi peke yake. Tungependa iajiri watu kutoka katika sehemu zote za Kenya kwa sababu tunawakilisha watu kutoka katika sehemu hizi zote katika Bunge hili la Seneti na pia la Kitaifa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}