GET /api/v0.1/hansard/entries/777394/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 777394,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/777394/?format=api",
    "text_counter": 77,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. King’ara",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika. Unajua huu ni wakati wa kutafuta uwiano, ndiyo maana unaona watu wanazungumza hapa na pale. Nasimama kuunga mkono hili jina la Prof. Hamadi Iddi Boga. Kulingana na matokeo ya kamati yetu teule ya Bunge tuliona ni mtu ambaye amesoma na kutembea maeneo mbalimbali. Hapa Kenya, kuna ukosefu wa utafiti katika kilimo. Kwa hivyo, tukipata mtu ambaye atatuelekeza kwa utafiti mwafaka, naona maendeleo na kilimo kitakuwa cha hali ya juu. Sisi Wakenya tunajigamba kuwa wakulima lakini hatuna chakula cha kutosha. Nchi yetu inaagiza chakula kingi sana kutoka nchi nyingine ilhali tuko na ardhi ya kutosha. Umuhimu wa kilimo ni kujitosheleza sisi wenyewe. Kwa hivyo, itabidi mwenzetu mteule aweze kuisaidia Kenya ndiyo tuweze kuuza chakula nje na sio kukiagiza kutoka nje. Akifanya hivyo, atakuwa amefanya kazi ambayo inastahili na inayolingana na masomo yote ambayo alisoma katika vyuo The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}