GET /api/v0.1/hansard/entries/777412/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 777412,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/777412/?format=api",
    "text_counter": 95,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Kuhusu Kamati ya Kilimo na Mifugo; kila wakati tukijaribu kutenga pesa kwa kilimo; mara kwa mara, unakuta pesa zinaenda pahali pengine. Naunga mkono Hoja hii nakusema ni muhimu tutenge pesa nyingi kwa sekta ya kilimo. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi iko na idara nyingi. Wafugaji wanaumia sana. Pesa ikitengwa kwa mambo ya mifugo, sisi ndio tunaumia. Ukame na njaa zinamaliza wanyama. Maji inategemewa kwa mambo ya wanyama. Kwa hivyo, tunaumia kabisa kama wafugaji. Kama sasa, kila mtu anaona katika Kenya vile mifugo wanakufa kwa sababu ya ukosefu wa maji na nyasi."
}