GET /api/v0.1/hansard/entries/777957/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 777957,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/777957/?format=api",
    "text_counter": 36,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadime",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2451,
        "legal_name": "Andrew Mwadime",
        "slug": "andrew-mwadime"
    },
    "content": "Asante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipatia fursa hii. Vile vile, watu wa Taita County, haswa Mwatate, wanaunga mkono malalamishi na kilio kuhusu wanyama pori, haswa vile wanaharibu mimea na kuua watu, lakini hakuna malipo yoyote. Kitu ambacho kimetushangaza zaidi ni kwamba watu wanabebeshwa mizigo juu ya mingine. Ndovu wanatolewa Laikipia na kupelekwa Mbuga ya Wanyama Pori ya Tsavo. Badala ya kumaliza hiyo taabu kule Laikipia, wanatupelekea hiyo taabu kule Taita. Tafadhali, tunaomba wakati mnaanaglia hili suala la malalamishi, jaribuni kuliangalia vyema. Tayari ukiangalia orodha ya malipo ya fidia Kenya nzima, wakazi wa Taita Taveta County ndio wanaodai hela nyingi zaidi. Sasa ndovu wanatolewa kwingineko na kupelekwa kule kwetu. Ni kilio kikubwa, tumepoteza watu wengi. Hivi sasa twafa njaa kwa sababu ya uharibifu wa mimea uliotekelezwa na wanyama pori. Hivi juzi niliwaelezea watu wangu kule Mwatate kwamba, Katiba inaruhusu wakati mumevamiwa na wanyama tafadhali, muleni ndiyo pengine KWS wataamka kidogo. Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa fursa hii."
}