GET /api/v0.1/hansard/entries/778062/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 778062,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/778062/?format=api",
    "text_counter": 141,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Tuwei",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13436,
        "legal_name": "Vincent Kipkurui Tuwei",
        "slug": "vincent-kipkurui-tuwei"
    },
    "content": "Balozi Macharia alitufurahisha sana alipotuahidi kutusaidia kupigana na janga la ufisadi. Alisema kwamba janga la ufisadi ni janga la ulimwengu mzima na kwamba wataalamu wakisimama imara na kuwe na mikakati katika Serikali, ama kuwe na uongozi bora; ufisadi utapungua. Pili, tulifurahi zaidi aliposema kwamba Wakenya wengi walioko katika nchi za nje wametaabika sana wakitafuta mawazo na mwongozo. Alisema kwamba akipata hii kazi ya katibu, atafanya juhudi kuona kwamba amewasaidia mabalozi ili Wakenya walioko katika nchi nyingine ulimwenguni waweze kujulikana mahali walipo, na pia waweze kujua sheria za nchi hizo kabla ya wao kuingia katika nchi hizo.Tatu, tulifurahia jibu alilotupa – kwamba mtu yeyote ambaye atacheza na Mkenya ataadhibiwa. Hilo ni jambo zuri ambalo litaifanya nchi yetu iheshimike ulimwenguni. Pia, jambo hilo litatuwezesha kufurahia nchi ambayo ina vijana walio na ujuzi utakaowawezesha kupata kazi katika nchi nyingine na kuleta pesa ambazo zitaisaidia nchi hii. Kwa hayo machache, ninaunga mkono kuteuliwa kwa Balozi Kamau kama katibu mkuu."
}