GET /api/v0.1/hansard/entries/779075/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 779075,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/779075/?format=api",
"text_counter": 431,
"type": "speech",
"speaker_name": "March 6, 2018 SENATE DEBATES 49 Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bi Spika wa Muda. Kwanza, ninatoa pole zangu nyingi kwa watu wa Mount Elgon, hususan watu wote wa Bungoma ambao wanaomboleza sasa hivi. Wataendelea kuomboleza kwa sababu tunaelewa ya kwamba hizi ghasia bado zinaendelea. Nampatia pole zangu ndugu na kiongozi wangu Seneta Wetangula. Macho yote yanamuangalia kama kiongozi katika Taifa la Kenya na kiongozi wa wachache katita Bunge la Seneti. Ni Mwenyezi Mungu ambaye hutupa maisha katika ulimwengu huu. Lakini kulingana na Katiba ya nchi hii, ni jukumu la Serikali kuhakikishia kila Mkenya usalama wa maisha yake. Hivi sasa tunaona ya kwamba Serikali haitekelezi wajibu wake ipasavyo. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba Waziri na Katibu katika Wizara ya Maswala ya Ndani na Taratibu za Serikali ya Kitaifa, Bw. Matiangi, alikuwa akiongea sana akiwa katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Wakati huu tunaona ni kama mdomo wake umefungwa; hasemi chochote. Ni kama haoni hii shida ambayo inakumba watu wa Mount Elgon. Hili si jambo la Mount Elgon pekee, bali nchi yetu hivi sasa imekumbwa na ghasia kila mahali. Kwa mfano, ukiangalia Kaunti ya Lamu, wanasema kuwa ni magaidi wa Al Shabaab ambao husababisha maafa. Kule Mount Elgon wanasema ni Saboat Land Defence Force (SLDP). Haya matukio yanafanya sisi kujiuliza maswali kadha: Je, Serikali hii iko na polisi na wanajeshi wa aina gani? Je, viongozi wake wanazembea kazini? Ni jukumu la Serikali kutetea maisha ya kila mwananchi anayeishi katika nchi hii. Kuna shida za kiusalama katika miji ya Lamu, Malindi, Kilifi na Kwale. Watu wengi wamepoteza maisha na mali yao kuharibiwa. Ni maombi yetu Serikali iamke na iweze kuchukua hatua mwafaka ya kuhakikisha maisha na mali ya raia wake inalindwa. Bi. Spika wa Muda, tunaona ya kwamba vijana ambao tunapeleka kwa mafunzo ya polisi na pesa zetu za ushuru hawawezi kuaminiwa. Siku hizi ukienda kutoa ushahidi na useme kuwa uliona kitendo fulani kikitendeka, basi ujue pia chuma chako kimotoni. Hii ni kwa sababu askari huyo umeenda kumripoti kwake ndiye anaweza kuwaambia majambazi kuwa uliripoti kushuhudia tukio fulani. Kwa hivyo, wajue kwamba mtu fulani ameshaenda kuwaripoti. Mwisho, ninasisitisha kuwa ni jukumu la Serikali kuona ya kwamba maisha ya kila Mkenya anayeishi humu nchini yamelindwa vilivyo. Asante sana, Bi Spika wa Muda."
}