GET /api/v0.1/hansard/entries/779084/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 779084,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/779084/?format=api",
    "text_counter": 440,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi Spika wa Muda. Kwanza, ningependa kuchukua fursa hii kutuma rambirambi zangu pamoja na zile za watu wa Mombasa kwa watu wa Mlima Elgon na Bungoma, kwa mkasa huu wa mauaji ya kiholela ya watu thelathini, wakiwemo watoto, kina mama na wasichana ambao hawakuwa na hatia yoyote. Bi Spika wa Muda, ni jukumu la Serikali kulinda maisha na mali ya Wakenya au watu wowote walioko nchini Kenya. Hilo ni jukumu ambalo tungependa kulisisitiza kwa sababu tumeona kumekuwa na utepetevu kwa Serikali kuhusiana na usalama wa wananchi na mali yao. Juzi tumeona katika Kaunti ya Bungoma, kila usiku na kila uchao, watu wanauawa na polisi wanasema, “Tunachunguza.” Watu thelathini wamekufa na wao bado wanachunguza; watachunguza mpaka lini? Hivi majuzi, tuliona hapa jinsi walivyotumia rasilimali zote za polisi kuhakikisha kwamba Miguna Miguna The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}