GET /api/v0.1/hansard/entries/779086/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 779086,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/779086/?format=api",
    "text_counter": 442,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "amefurushwa kutoka nchini Kenya, ilhali watu masikini walioko majumbani mwao hawawezi kuhakikishiwa usalama ili waishi na familia zao bila matatizo. Bi Spika wa Muda, kuna suala la usalama katika kaunti – ijapokuwa serikali za kaunti hazina jukumu hili – lakini kuna suala la County Community Police Committee . Hiki ni kitengo kimoja kinachoweza kutumika kusaidia polisi kuhakikisha kwamba kuna usalama katika hizi kaunti. Hadi sasa, Inspekta Mkuu wa Polisi hajaanzisha hizi kamati za usalama wa jamii katika kaunti zote nchini Kenya. Vile vile, hajatoa utaratibu ama muongozo wa kufuatwa kuhusu kamati hizi zitaundwa vipi na zitafanya kazi vipi na polisi ili kuhakikisha kwamba usalama unadumishwa. Kitengo kingine ambacho kimelala katika ngazi za polisi ni kile cha ujasusi. Itakuwaje watu wanauawa kila usiku katika eneo moja bila ya polisi kujua hawa wanaoua ni kina nani na ni kwa nini wanaua? Imefikia hadi familia 30 zimepoteza wapendwa wao na bado tunaendelea kuhesabu, lakini makachero wa polisi bado hawajatoa mwelekeo kuhusu ni kina nani wanaoua na ni kwa nini wanaua. Tumeaona kwamba ijapokuwa Serikali na nchi imechukua muda mrefu kujaribu kuleta mabadiliko katika jeshi la polisi, tunaona kuwa jinsi mambo yanavyobadilika, ndivyo yanabakia vilevile yalivyokuwa. Bi Spika wa Muda, suala la Sabaot Land Defence Force (SLDF) katika Mlima Elgon ni jambo lililopita wakati wa nyuma. Ni juzi tu katika mwaka wa 2007/2008 ambapo kikosi au maharamia wa SLDF walipokuwa wanahangaisha watu katika maeneo ya Mlima Elgon. Miaka sita au saba baadaye, tatizo lile lile limerudi. Hii inamaanisha kwamba Serikali haijakuwa macho na haijazingatia kwamba maisha ya binadamu ni muhimu katika nchi ya Kenya. Kwa hivyo, naomba kwamba zile"
}