GET /api/v0.1/hansard/entries/780103/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780103,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780103/?format=api",
    "text_counter": 148,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "March 13, 2018 SENATE DEBATES 19 Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika . Uvuvi ndio rasilimali kubwa kwa watu wa Pwani, kutoka Kiunga, Kaunti ya Lamu mpaka Vanga katika Kaunti ya Kwale. Kutokuwepo kwa taasisi maalumu ya kuangalia mambo ya uvuvi imeleta hasara kwa sababu trawlers zinazo milikiwa na wageni kutoka nchi za nje zinapata fursa ya kuingia na kuiba samaki wetu. Hali hiyo inasababisha upungufu wa samaki. Ningependa kukubaliana na Sen. Kajwang’ kwamba taarifa ilioletwa bungeni alasiri ya leo hairidhishi. Tunafaa kuunda tume ama mkutano wa stakeholders katika mambo ya uvuvi ili rasilimali yetu ya uvuvi isiende bure. Bw. Spika, sehemu ya Kiunga mpaka Vanga ni kubwa sana, ilhali hakuna patrols za kuweza kuzuia uvuvi kutumia trawlers ambazo zinatoka nje ya nchi. Vile vile, kwa sasa, ili mtu apate leseni ya uvuvi inabidi aje Nairobi ilhali uvuvi ni sekta ambayo imekuwa- devolved kwenye kaunti. Jambo hili linaongeza corruption. Sio sawa kumlazimisha mtu kusafiri kutoka Mombasa au Lamu kutafuta leseni ya uvuvi kwa sababu atagharamika kusafiri na kulala ilhali leseni inaweza kupatikana sehemu yoyote katika Jamhuri ya Kenya. Bw. Spika, namuunga mkono Mhe. Kajwang’ kwa maelezo aliyotoa."
}