GET /api/v0.1/hansard/entries/780488/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780488,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780488/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadime",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2451,
"legal_name": "Andrew Mwadime",
"slug": "andrew-mwadime"
},
"content": "Ninakumbuka nilipotoka chuoni nilienda kufundisha mahali ambapo nilikuwa natofautiana napo kitabia na masuala mengi tu. Baada ya muda mfupi tumbo lilianza kuwa na vidonda. Muda kidogo nilikuta risasi ambayo kwa Kiingereza inaitwa stray bullet ikanigonga na maisha yangu hayakuwa sawa sawa. Mwalimu ambaye maisha yake hayako sawa sawa kufundisha ni uongo. Hapo tunadanganyana. Ni vizuri TSC iangalie suala hili kwa undani. Pia tunafahamu kwamba hapa Kenya ukabila upo. Hivi sasa ukienda kule utakuta kuwa wale wako huko ambao si jamii ya huko ni wale watu wadogo wadogo ndio wamesukumwa huko. Hao ambao wanapitisha sheria hizo watoto wao wako katika shule za mijini na kila mahali. Ingekuwa hao wanawapeleka watoto wao huko ingekuwa ni vyema zaidi. Saa hii ninapoongea, kuna kijana anayetoka kule kwangu ambaye hana baba wala mama. Tangu mwaka juzi amekuwa akilia akisema: “Mheshimiwa, mimi nina ndugu zangu wadogo. Hii kazi kidogo angalau nimepata nafundisha huko. Mimi sijazoea masuala ya mabundiki. Nataka kuja huko nyumbani ama kwengineko kule Kenya.” Hamna. Nimejaribu lakini ni tatizo. Watu wasichukulie suala hili hivi hivi. Waliangalie kwa kina kabisa. Kama walimu ambao wako kule hawasikii kufanya kazi kule wapatiwe nafasi kwani nafasi ziko nyingi Kenya nzima. Vile vile, suluhu mwafaka itafutwe maana wale watoto ni wetu pia. Hatutaki wakose masomo kule Mandera na unajua wakati hakuna masomo ndio basi bunduki zitalia zaidi huko. Kwa hivyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu na Utafiti, ningeomba uyaangalie malalamishi haya kwa undani kabisa. Angalia pande zote ili tupate suluhu mwafaka tuone jinsi watoto wa kule watakavyosaidika na wale ndugu zetu ambao wako kule wanalia watasaidiwa namna gani. Nikikumbuka, yale niloyoyaona 1990 hayakuniridhisha. Najua wengi wenu hapa wakati huo mlikuwa hamjamaliza chuo. Yale niliyoyaona yalikuwa mengi. Ilinibidi nipeleke mashtaka dhidi ya Wizara ya Elimu kule kortini. Kwa bahati mbaya walinishinda na nikaumia sana. Niliomba msamaha ndio nikarejea maana nilikuwa sina namna."
}