GET /api/v0.1/hansard/entries/780613/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780613,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780613/?format=api",
"text_counter": 37,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamend Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, hili ni wazo ambalo liliwahi kuletwa na Rais Uhuru Kenyatta Juni mwaka uliopita. Rais alipendekeza kwamba katika kila kaunti, kuwe na hospitali ya rufaa. Ningependa kutoa utaratibu wa mambo fulani ambayo yanachangia kuwepo kwa hospitali hizi kwa sababu asilimia 80 ya Wakenya ni wale ambao hawawezi kufikia huduma hizi za afya. Nitaanza kwa kutoa mifano ambayo imesalia katika historia ya Kenya. Nitaanza na kwangu nyumbani kule Mombasa. Kuna mtoto mdogo kwa jina la Satrin Osinya au Baby Osinya aliyepigwa risasi na akakaa na risasi kichwani kwa takriban siku nne kabla ya kuletwa Nairobi ili afanyiwe upasuaji. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba iwapo hatutakuwa na huduma za afya katika kila kaunti, basi tutakuwa katika hali mbaya sana. Hospitali ya Coast General iliyoko Mombasa inahudumia kaunti sita ambazo zinajumuisha Taita Taveta, Tana River, Kwale na Kilifi. Hizi ni baadhi ya kaunti ambazo zinategemea hospitali hii katika huduma za rufaa. Shirika la Afya Duniani (WHO) lina mapendekezo yake ambayo yanasema kwamba daktari mmoja anafaa ahudumie wagonjwa elfu moja lakini hapa nchini Kenya, daktari mmoja anahudumia wagonjwa elfu kumi. Hili ni jambo ambalo haliwezekani, si la msingi na haliingii akilini. Tangu tupate Uhuru miaka 55 iliyopita, tuna hospitali mbili peke yake ambazo ni hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na ile ya rufaa ya Eldoret."
}