GET /api/v0.1/hansard/entries/780615/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780615,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780615/?format=api",
"text_counter": 39,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamend Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": "Mhe. Spika wa Muda, nadhani utashangaa nikikwambia ya kwamba taifa hili lina madaktari wa kutibu saratani yani oncologists, kwa lugha ya kimombo wanaohudumia Wakenya takriban 45 milioni madaktari 23 peke yake. Hawa madaktari ni wa kibinafsi. Namaanisha nini? Wanahudumu katika hospitali ambazo ni za wale ambao wana nguvu kama Aga Khan University Hospital na Nairobi Hospital. Mkenya wa kawaida hawezi kuenda kutibiwa ugonjwa wa saratani katika hospitali hizo. Miaka 55 imepita tangu Kenya ipate Uhuru na tunajipiga kifua tukisema tumeendelea, na ilhali tuna madaktari wa upasuaji yaani neurosurgeon 18. Hii ni aibu iwapo tuna madaktari 18 Kenya nzima. Leo tunajipiga kifua na kusema ya kwamba tuna madaktari tosha ambao ni wa figo, kwa lugha ya kimombo tunawaita nephrologists . Hawa ni 16 peke yake. Mombasa tuna wawili pekee. Ni nani atawafikia hawa maskini?"
}