GET /api/v0.1/hansard/entries/780616/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780616,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780616/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamend Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": "Leo Mbunge katika Bunge hili akisikia anasokotwa na tumbo kidogo tu, yeye ana daktari wake wa kipekee. Yeye ana nguvu za kwenda katika hospitali na kuhudumiwa mara ya kwanza. Kule mashinani, kuna watu ambao tumbo zao zinanguruma kama mitambo ya kuchapia mahindi lakini hawajui wataenda wapi, kwa sababu hawana daktari wa kibinafsi, hospitali haziko karibu na iliyoko karibu iko katika kaunti nyingine. Haya ndiyo mambo ambayo nataka tuangalie. Kwa mfano, Kenya nzima madaktari waliosomea taaluma mbalimbali ambazo nimezitaja kama vile saratani, upasuaji na figo ni 425. Nitakupatia utaratibu tu wa kukuonyesha athari ambazo zinaweza kutupata iwapo hatutaweza kushughulikia janga hili, na kupitisha Hoja hii na kuhakikisha kwamba hospitali zimeweza kufika katika kaunti. Nitakupa mfano wa kaunti ya Mombasa ambayo idadi yake ni watu 939,370. Madaktari wanaohudumia watu hawa takriban milioni moja ni 198. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}