GET /api/v0.1/hansard/entries/780617/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 780617,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780617/?format=api",
    "text_counter": 41,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mohamend Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13455,
        "legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
        "slug": "mohamed-ali-mohamed"
    },
    "content": "Katika kaunti ya Kwale, watu 649,331 wanahudumiwa na madaktari 65. Hawa ni watu takriban 700,000. Sehemu kama Nyeri ambayo ina watu takriban 700,000 wanahudumiwa na madaktari 143. Kiambu ambayo ina watu takriban 1.6 milioni wanahudumiwa na madaktari 278. Kisumu ambayo idadi yake inakaribia milioni moja, wanahudumiwa na madaktari 163. Ukiangalia kaunti ya Kisii ambao ina idadi ya 1.2 milioni wana madaktari 163, utaona ya kwamba wanahitaji madaktari 989 zaidi. Kisumu wanahitaji madaktari 800. Kiambu wanahitaji madaktari 1,343. Hizi tu ni baadhi ya sehemu ambazo zinaathiriwa sana. Hii ndiyo sababu ambayo imetuleta katika Bunge hili. Tulienda kupiga kampeini na tukawaahidi wananchi ya kwamba tutakuwa sauti yao katika Bunge hili. Tulitoa ahadi zote. Nadhani ahadi ambayo tutaitoa kwa Wakenya na ambayo itasalia mioyoni mwao ni ya kuhakikisha katika kila kaunti katika taifa hili kuna hospitali ya rufaa na mwananchi wa kawaida ataweza kuhudumiwa."
}