GET /api/v0.1/hansard/entries/780621/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780621,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780621/?format=api",
"text_counter": 45,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamend Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": "Nitaendelea bado kwa kueleza ni kwa nini hasa tunataka hizi hospitali ziweze kuhudumia wananchi. Nitaanza na masuala ya rufaa. Leo mgonjwa akiwa Nyeri, Kiambu, Mombasa ama Turkana, ataenda katika hospitali iliyoko hapo. Hospitali za maskini ni hospitali za Panadol, dawa ya maumivu tu, maana hawana dawa zingine. Wakienda katika hizi hospitali, iwapo wana kesi nyeti, ni lazima waletwe Nairobi. Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta ina madaktari 264. Wale ambao wanasimama pale casualty kwa matibabu ya dharura ni sita. Kwa mfano, Hospitali ya Coast General inapokea zaidi ya watu 50 kwa siku moja kutoka kaunti mbalimbali waliotumwa kwa sababu vifaa ama huduma inapatikana huko. Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta inapokea kati ya watu 200 na 300 kila siku kutoka sehemu mbalimbali sawia na ile ya Eldoret."
}