GET /api/v0.1/hansard/entries/780622/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 780622,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/780622/?format=api",
"text_counter": 46,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mohamend Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13455,
"legal_name": "Mohammed Ali Mohamed",
"slug": "mohamed-ali-mohamed"
},
"content": "Mwaka wa 2015/2016, Serikali ya Kenya ilitumia Kshs.38bilioni kwa mashine za kisasa katika hospitali lakini kwa sasa hazifanyi kazi, kwa sababu hatuna madaktari wanaopata mafunzo ya kuzitumia. Mwaka uliopita 2015/2016, iliangaziwa katika vyombo vya habari ya kwamba mashine za kisasa za saratani na figo zimekuja. Watu walifurahi na wakasema kweli ugatuzi umezaa matunda. Ugatuzi wakuleta mashine bila daktari wa kujua kuzitumia nikutia gunia upepo kwa maana haina faida. Ninaposema kutia gunia upepo na maanisha ya kwamba unatia gunia upepo lakini linatoa. Kwa hivyo, haujazi. Inakuwa ni kazi ya bure. Je, kujenga hospitali moja ya rufaa katika kaunti moja itagharimu Serikali pesa ngapi? Itagharimu takriban Kshs3bilioni. Tukisema tuboreshe zile zilizopo ambazo nimezitaja kutoka Level 5 hadi Level 6, tunaweza tumia Kshs2bilioni. Sasa wacha nikupe mfano tufanye hesabu. Kujenga hospitali moja ni Kshs3bilioni. Kuboresha hospitali iliyoko ni takriban Ksh2bilioni. Idadi ya Wakenya wanaondoka nchini kuenda kutafuta matibabu nje hususan taifa la India, kila mwaka wanatumia Kshs10bilioni. Ni jambo linaweza kufanyika. Idadi ya watu wanaokufa inazidi kuongezeka. Mungu ametujalia tumeletwa katika Bunge hili kujadili na kutunga sheria, lakini hatutungi sheria ambazo zitatulinda pia sisi tukitoka, maana hakuna mtu atakayeishi hapa milele. Tukitoka hapa, vizazi vyetu hatujui kama vitakuwa vya ubunge, kula madawa ya kulevya ama kuiba. Watakuwa ni miongoni mwa wale ambao watapata matatizo ambayo sisi tunasuluhu sasa hivi. Nitakupa mifano nikianzia na mgomo uliofanyika miezi minane iliyopita, wakati madaktari waligoma. Nitakupa tu mifano na kaunti kadhaa kama Kaunti ya Kilifi. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposes only. Acertified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}